Wednesday, April 9, 2014

Misri nayo ya moto wa kuotea mbali kwa mashoga.

Vurugu na myumbo nchi Ukraine, Marekani yaishutumu Urusi.

Washington, Marekani - 08/04/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameishutumu serikali ya Urusi kwa kuendeleza mvurugo na myumbo wa kisiasa nchi Ukraine ambao unapelekea kugawa nchi.

Akiongea mbele ya wajumbe wa Kongresi John Kerry amesema kuwa '' mashushu, makachelo na maafisa usalama wa Urusi wapo nchi Ukraine kusaidia kuyumbisha serikali iliyopo na kuunga mkono wale wote wanao taka mgawanyiko wa nchini Ukraine.''

'' Ushaidi ni kwamba watu ambao wamevamia na kuchukua majengo ya serikali ni wale ambao wanaunga mkono kujiunga na Urusi na na pia kujitenga na serikali ya Kiev, na hii inatokana na ushawishi wa Urusi.''

Hata hivyo serikali ya Urusi imekuwa ikipinga  kwa kudai kuwa vurugu na myumbo wa kisiasa nchi Ukraine umesababishwa na ya Marekani na washiriki  kutokana na malengo na faida wanazojua wenyewe.

Mvurugona wa kuchafuka kwa amani   nchini Ukraine umekuwa  wa kichwa kuuma, tangu kuangushwa kwa serikali ya rais Viktor Yanukovich  ambapo nguvu na maandamano yalitumika na vyama vya upinzani chini Ukraine kwa msaada wa msukumo wa nchi za Ulaya Magharibi na Marekani.na kuleta upya hisia za vita baridi kati na Urusi.

Hadi sasa majimbo ya Donetski na  Kharkiv yamekumbwa na maandamano ya  kutaka kujitenga na serikali ya Kiev, pia baadhi ya watu waliovamia ofisi na majengo ya serikali kudai majimbo hayo yajiunge na Urusi.

Polisi nchini Kenya yasaka wahamiaji haramu.

Nairobi. Kenya - 08/04/2014. Polisi nchi Kenya wapo katika msako mkubwa  kuwakamata watu wote wanao ishi kinyume cha sheria nchini Kenya baada ya matukio ya  mashambuzi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa nchi humo.

Katika kufanikikisha zoezi hilo wagtu 4,000 walikamatwa katika jiji la Nairobi, japokuwa polisi wamesema '' ni watu 447 ambao kwa sasa ndiyo bado wanashikiliwa na polisi.''

Kwa mujibu wa balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Shaik Ali '' watu 82 wamerudishwa nchini Somalia baada ya kukataliwa maombi yao ya kikimbizi.''

Hatua hii ya serikali ya Kenya kufanya msako imekuja baada ya kutoa agizo kuwa watu wote walioomba ukimbizi  kurudi katika makambi ya kikimbizi.

 Agizo hilo lilikuja baada ya shambuli lililotokea katika maeneo ya Elselegh ambapo watu sita walipoeteza maisha kufuatia mashambulizi ya mabomu katika kumbi za starehe kwenye kitongoji hicho.

Kenya imekuwa inakutwa na mashambulizi ya kigaidi, baada ya kundi la Ashabab la Somali kudai kuhusika na ugaidi nchini humo kwa madai yakuwa Kenya imevamia nchini Somalia, jambo ambalo serikali ya Kenya inasema ni katika harakati za kuleta amani katika ukanda wa pembe ya Afrika.

Misri nayo ya moto wa kuotea mbali kwa mashoga.

Kairo, Misri -09/04/2014.  Watu wanne wamehukumiwa kwenda jela na mahakama jijini Kairo, baada ya  kutwa na hatia ya kufanya ushoga na kuwa kimapenzi kwa jinsia moja.

Watu hao ambao wamekutwa na kosa la kupanga na kushiriki kwa makusudi sherehe ya ushoga huku wakiwa wamevaa nguo za kike na ulimbwende wa kina mama walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minane na kupewa kazi ngumu wakati wa kipindi chote watakachokuwa jela.

Kufuatia hukumu hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la kutoka Marekani limelaani kitendo hicho na kwa kusema '' kitendo cha kufungwa watu hao ni kimyume za haki za binadamu na kitaleta mlolongo wa hukumu kama katika nchi zenye asili ya  Kiarabu.''

Nchi ya  Misri haina sheria ya kupinga ushoga, lakini mashoga na wale wote wanahusika na tabia hii huwa wanahukumiwa kwa kufuata baadhi ya vifungu ungia vya sheria .

Nchi nyingi za Afrika zimekuwa hazikubaliani na tabia ya ushoga, na hivi karibuni serikali ya Uganda ilipitisha sheria kali ya kupinga ushoga jambo ambalo  nchi za Magharibi zililaani sheria hiyo na pia kutishia kusimamisha baadhi ya misaada kwa Uganda.


Tuesday, April 8, 2014

Mwanajeshi wa Ufaransa atia chumvi kidonda cha kuhusika na mauaji ya Rwanda 1994.

Mwanajeshi wa Ufaransa atia chumvi kidonda cha kuhusika na mauaji ya Rwanda 1994.Paris, Ufaransa - 08/04/2014. Mmoja wa makamanda waliokuwa katika kikosi cha kijeshi cha Ufaransa kilichokuwa nchi Rwanda wakati wa mauaji wa kimbari ametoa changamoto kwa serikali jiji Paris juu shutuma kutoka kwa serikali ya Rwanda.

Guillaume Ancel ambaye alikuwa kapteni  katika jeshi la Ufaransa jiji Kigali mwaka 1994 kabla  mauaji ya kimbari kuanza amesema '' niliamliwa kupakia siraha katika roli ili ziende Zaire au kwa sasa Kongo DRC na zilikuwa kwa ajili ya askari wa Rwanda ambao watakimbia na ndiyo walikuwa wahusika katika mauaji ya kimbari''

''Pia nilishauriwa kuhakikisha waandishi wa habari wasijue, na nilipo pinga swala hili niliambiwa kuwa ikiwa kama hatutashirikiana na jeshi la Rwanda la wakati hule, basi watatugeuka na tutakuwa katika hali ya mvutano nao.''

''Na hii ilitokea baada ya mauaji ya kimbari ya 7/April/1994 na  ndege iliyombeba rais  wa Rwanda Juvenal Habyalimana kuangushwa katika kiwanja cha ndege cha Kigali.''

''Kwangu nilishangaa kwa  kutokuelewa kuwepo kwa jeshi la Ufaransa kwani tayari jeshi la Umoja wa Mataifa UNAMIR lilikuwa tayari mjini Kigali.'' Aliongezea Ancel.

Tangu kutokea mauaji ya kimbari  ya mwaka 1994 nchini Rwanda, serikali ya  Rwanda chini ya rais Paul Kagame imekuwa ikizishutumu Ufaransa na Ubeligiji kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari, ambapo watu baadhi ya watu wenye itikadi kali toka jamii ya Kihutu  waliwaua watu 800,000 wa jamii ya Kitutsi na huku waangalizi  wa umoja wa mataifa wakiwa wapo na butwaa.

Monday, April 7, 2014

Rais Paul Kagame awakalia kidede waliohusika na mauaji ya kimbari.

Rais Paul Kagame awakalia kidede waliohusika na mauaji ya kimbari.

Kigali, Rwanda - 07/04/2014.
Wanachi wa Rwanda wameadhimisha kumbumbu  ya mauaji ua kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuwawa katika mauaji ambayo yalichukua zaidi ya siku miamoja.

Rais Paul Kagame, akilihutubia taifa katika kuadhimisha siku ya mauaji ya kimbari amesema " japokuwa muda umepita ukweli upo katika historia ambayo ipo na itajiandika, kwani watu au nchi hawawezi kuhonga au kulazimisha kubadirisha historia japo wawe na nguvu au kuwa nguvu kwani ukweli upo wazi"

" Na miaka 20 sasa cha muhimu ni  kuwa hawa kuwa na imani ya kusimamisha mauaji ya Wanyarwanda na wanachofanya ni kukanusha."
 "Wanyarwanda wanatakiwa kujua uhai na thamani ya mtu ambayo wenzetu hawajui nini maana yake na kuitumia vibaya."

Kabla ya kuhutubia, rais Kagame mbele wa wageni waalikwa aliwasha mwenge wa amani  ambao utakimbizwa kwa kuzungushwa nchi nzima kwa muda wa siku 90 ikiwa ni ishara ya kukumbuka siku ambazo mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994. 

Rais Paul Kagame amekuwa akizilaumu  Belgium na Ufaransa kwa kuhusika na mauaji ya kimbari yaliyo tokea nchi Rwanda mwaka 1994 na kuzitaka nchi hizo kuwa za uwazi katika ukweli, kwani histotoria ya mauaji ya Wanyarwanda itakuwa nao daima japo nchi hizo zimekuwa zikikanusha kuhusika na mauaji hayo.

Aliyekuwa rais wa Pakistani anusurika Kifo.

Rawapindi, Pakistan - 07/04/2014. Aliyekuwa rais wa Pakistani na ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya uhaini ameponea chupu chupu na jaribio la kutaka kumwua ambalo lilifanyika hivi karibuni.

Pervez Musharraf alipona hali hiyo ya kutaka kuuwawa baada ya bomu kulipuka katika daraja lililopo njia ambayo muda mchache Musharraf alitakiwa kuitumia kuelekea katika kambi ya jeshi iliyopo Rawapindi ambapo alitakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Musharafu ambaye kwa sasa anaishi nje kidigo ya jiji la Islamabadi alielekea hospital kwa kutumia njia nyingine ambayo ilikaguliwa na walinzi wake.

Kupona huko kwa Pevez Musharraf kumekuja  kwa mara ya pili, baada ya  bomu kulipuka Desemba  2003 katika maeneo ya Rawapindi baada ya msafara wake kupita katika eneo ambalo bomu lilikuwa limetegwa  na kumkosa kwa dakika chache.

Kundi la Taliban limekuwa likihaidi kumwua kiongozi huyo, ambaye alichukua madaraka kwa nguvu za kijeshi mwaka 1999 na baadaye kuwa rais tangu mwaka 2001 -2007.

Rais Assad atuma salamu kamambe  kwa rais wa Urusi.

Damascus, Syria - 07/04/2014. Rais wa Syria amefanya mazungumzo na aliyekuwa waziri mkuu wa Urusi Sergi Stepashin na kujadili ni kwa jinsi gani nchi hizo zitazidi kushikiana.

Rais Bashaar al Assad katika mazungumzo hayo alisema  " naomba kamwambie Vladmir Vladimirovich Putin kuwa mimi  nipo na sitaondoka kama alivyo ondoka rais wa Ukraine Viktor Yanukovich"

"Na hii hali ya kivita tutaimaliza na kushinda, kwani serikali yangu ipo imara na kupambana na  magaidi wanaodhaminiwa na wapinzani wenye nia mbaya na Syria kwa tamaa zao."

 Sergi Stepashim ambaye alikuwa waziri mkuu wakati wa utawala wa  rais Boris Yeltsin amesema " Assad  inaungwa mkono na watu wengi nchi Syria na hata kama kura zikipigwa leo atashida"

" Na kwa kuwa anataka kugombania uchaguzi ujao basi naimani atashida kwa kura nyingi bila shida"Alimalia Sergie Stepashin.

Urusi imekuwa nchi ambayo inaungana mkono serikali ya rais Assad, ambaye kwa sasa nchi yake ipo katika vita ambavyo vimeanza zaidi ya miaka miwili kati yaserikali na makundi ya upinzani ambayo inasadikika kuungwa mkono na badhi ya nchi za Magharibi  na nchi za Kiarabu na huku majeshi ya Assad yakiungwa mkono na kundi Hezhibollah.

Saturday, April 5, 2014

Rwanda yatimiza miaka 20 tangu mauaji ya kimbari.

Rwanda yatimiza miaka 20 tangu mauaji ya kimbari.


Rwanda chini ya Uongozi wa rais Paul Kagame imekuwa na amani na maendeleo.

Kigali Rwanda - 05/04/2014. Wananchi wa Rwanda wameadhimisha miaka ishirini tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuwawa kutokana na chuki za kijamii zilizo zilizo sambazwa na kukuzwa katika jamii nzima ya Wanyarwanda.

Mauahi hayo yalitokea wakati watu wa jamiii ya Kihutu walipowauwaa watu wa jamiii ya Kitutsi jambo ambalo lilifanya dunia nzima kushikwa na butwaa kwa kuto kuamini na huku maelfu ya Wanyarwanda wakikimbia nchi yao katika kipindi chote cha mauaji hayo.

Akiongea katika kuadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji haya, rais wa Rwanda Paul Kagame amesema " jumuiya ya kimataifa na hasa Ufaransa zinatakiwa kulaumiwa kwa kuachia mauaji hayo kutokea."

Serikali ya rais Kagame imekuwa imara katika kuhakikisha kuwa historia hii haitarudia tena nchi Rwanda kwa kupitisha sheria kali ambazo zinazuia chuki katika jamii ya Wanyarwanda. na vile vile serikali ya Rwanda imehakikisha kuwa huduma za elimu. afya na nyingine muhimu zinapatikana kwa kila mtu aishiye katika nchi hiyo.

Mauaji ya Rwanda yalitokea mwaka 1994 na kuwa ya kihistoria katika bara la Afrika kwa jamiii moja ya wwtu kutaka kuifuta jamii nyingine ya watu kwa kuwauwa kwa sababu za chuki za kihistoria.

Askofu mkuu wa Anglikani atahadhalisha kuhusu ushoga.

London, Uingereza - 05/04/2014. Askofu mkuu wa kanisa la Anglika ameonya kuwa  ikiwa kanisa hilo litaruhusu ndoa za mashoga huenda likawa na wakati mgumu na idadi kubwa  waumini wake.

Askofu Justin Welby alisema " Kwa kiasi kikubwa waumini wa kanisa la Anglikani wapo katika bara la Afrika  na wakristu  ambao wamekuwa wakidhurika ni wale ambao wanaunga mkono maswala ya kishoga."

" Na hii inaweza kutokea ikiwa kanisa litapitisha sheria ya kuruhusu mashoga."

Akiongezea Askofu Welby amesema kuwa  wakuu wa kanisa hilo  nchi Sudani ya Kusini wamemwomba kutokubadirisha misingi ya kanisa, kwani "kiwa itatokea kubadirishwa basi waumini wa Sudani ya Kusini hawata kuwa na ushirikiano na kanisa la England."

Askofu Justin Welby aliyasema haya baada ya kumaliza ziara yake kutembelea bara la Afrika ili kujione nini kinatakiwa kifanyike ili kukuza imani ya waumini wa kanisa la Anglikani katika bara hilo.

Friday, April 4, 2014

Matumizi ya mtandao yatonesha kidondo cha Marekani na Kuba.

Makao makuu ya EU yawa kiwanja cha mapambano.


Brussels, Ubeligiji - 04/04/2014. Polisi katika jiji la Brussels wamepambana na waandamanaji wanao pinga mbinyo wa  matumizi  na mapato yaliyopo katika nchi za jumuiya ya nchi za wanachama wa Ulaya 

Wakitumia majiwasha na mabomu ya kutoa machozi, polisi waliwatawanya wanadamanaji waliyo kuwa katika maeneo ya ofisi za nchi za jumuiya wa umoja wa Ulaya,huku wengi wao walikuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi tofauti vilivyopo katika nchi za hizo.

Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yanayo kosoa mwenendo mzima wa mbinyo wa matumizi na uwekezaji  ambao uongozi wa nchi za jumuiya ya Ulaya umekuwa ukikazania mbinyo huo kama njia pekee ya kuinua uchumi.

Mmoja wa kiongozi wa chama cha wafanyakazi ETUC, Emanuel Bonaciana amesema kuwa "nia ya maandamano ni kuwataka  viongozi kuja na njia mbadala ya kukuza uchumi kwa kuwekeza na ajira iliyo sawa na haki kwa wote."

Hali ya mbinyo wa matumizi na uwekezaji, umeleta hali ya mstuko kwa wananchi wa nchi za jumuiya ya Ulaya na kulaumu kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa walio wengi na wachache ndiyo wanaoifaidika na mpango huo  na hasa mabenki.

Matumizi ya mtandao yatonesha kidondo cha Marekani na Kuba.Havana Kuba 04/04/2014.  Serikali ya Kuba imeilalamikia Marekani kwa kutumia mtandano unao fanya kazi kama  Twita ili kuaandaa mapinduzi nchini Kuba.

Msemaji wa serikali ya Kuba alisema kuwa mtandaa huo ambao una matumizi sawa na twita ulikuwa unalengo la kuhimiza wananchi wa Kuba kupingana na "serikali ya Kuba kwa kuwa ni ya kikomunisti"

Hata hivyo serikali ya Marekani imepinga kuhusika na njama hizo zakuhimiza wananchi wa Kuba kupingana na serikali yao, bali Marekani imekubali kuwepo na mtandao huo kama twita ambao ulikuwana madhumini ya kuwasaidia wa Kuba katika mawasiliano na ujenzi wa demokrasia.

Msemaji wa serikali ya Marekani Marie Harf amesema kuwa "hii siyo siri kwani mradi huo ulikuwa na nia ya kuweka uwazi ukuzaji wa demokrasia na ulikuwa wa miaka mitatu ambapo ulighalimu dola za $1.2 millioni na ulipitia na kudhaminiwa kwa kutumia wakala tofauti"

" Na hatukusambaza maswala ya kisiasa" Alimaliza Marie Harf.

Hata hivyo shirika la habari la AP limeripoti kwa kusema " mradi huu ulibuniwa kuzunguka vikwazo vya kimtandao vilivyo wekwa na serikali ya Kuba kwa kutumia makampunu yenye ubia na shell chini ya uongozi wa USAID shirika ambalo huwa linatoa misaada kwa masikini duniani"

Mzozo wa Kuba na Marekani ni wamuda na kuwa ni moja ya mzozo baridi ambao unaanzia 1962 na kupelekea Marekani kuwa na vikwazo na Kuba tangu kipindi hicho.

Wapalestina na Waizrael wampa kichwa kuuma John Kerry.

Rabat, Moroko - 04/04/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amesema kuwa kuna nia kubwa ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya kati ya Waizrael na  Wapalestina japo kwa sasa  kuna ugumu umejitokeza.

Waziri John Kerry aliyaongea hayo mjini Rabat Moroko, kwa kusema kuwa "hali ya mazungumzo yakuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina inahitaji kuangaliwa kwa njia zote za umakini kwa kuzingatia kwa sasa pande zote mbili simechukua hatua ambazo zinaleta ugumu wa kuendeleza mazungumzo ya kuleta amani."

Kutamka kwa waziri John Kerry kuhusu ugumu wa mazungumzo ya kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael kumekuja baada ya Uingozi wa Wapalestina  kusaini kwa pamoja kutaka kujulikana kama taifa , ambapo hapo awali ilikuwa ni moja ya makubaliano yaliyowekwa katika ya Izrael na Palestina.

Uongozi wa Palestina pia  umedai "Izrael imevunja mkataba wa makubaliano wa kuwaachi huru wafungwa wa Kipalestina waliopo katika jela za Kiizrael na kusitishwa kwa utanuzi wa ujenzi wa makazi ya Waizrael katika maeneo ya Wapalestina."

Hata hivyo kwa mijibu wa wachunguzi wa maswala ya amani ya mashariki ya kati wanadai kuwa kama "Kama serikali ya Izrael ingekubali kuaachia wafungwa wa Kipalestina, basi kungesababisha kuvunjika kwa serikali ya waziri mkuu Benyamin Netanyahu, jambo ambalo waziri Netanyahu limemletea ugumu kutimiza ahaadi ya kuwaachia wafungwa hao wa Kipalestina."

Mpango wa kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael umekuwa nawakati mgumu kwa muda mrefu  kwa serikali ya Marekani, jambo jitihada zimekuwa zikifanyika kwa hali na mali ili amani iwepo kati ya Wapalestina na Waizrael.

Saturday, January 18, 2014

Rais Yoweri Kaguta Museven awapa hafueni mashoga.

Rais Yoweri Kaguta Museven awapa hafueni mashoga.

Kampla, Uganda - 18/01/2014. Rais wa Uganda, Yoweri |Mseven, amkataa kusaini muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda.

Akiandika kupinga kwa sasa kutia sahii rais  Museven amesema " kweli ushoga si kitu cha kawaida na wanatakiwa kuokolewa na siyo kuhukumiwa."

Kitendo cha rais Museven kupinga kutia sahii muswada huo, kimetafsiliwa kuwa, ni kugopa msukomo wa kimataifa, ambapo ingepelekea kuleta mvutano kati ya serikali yake na mashirika ya kimataifa yanayo unga mkono ushoga ambapo mashirika hayo yanaushawishi mkubwa kimataia na kuweza kusababisha myumbo wa serikali ya Uganga kimataifa.

Thursday, January 16, 2014

Kesi ya Rafiki Hariri yaanza na kuhamishia masikio ya Walebanoni jijini Hague.

Kesi ya Rafiki Hariri  yaanza na  kuhamishia  masikio ya Walebanoni jijini Hague.

Hague, Uhollazi - 16/01/2014. Mahakama maalumu inayoshughulikia kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanoni Rafiki Hariri imeaanza rasmi jijini Hague Uhollanzi ambapo watu wanne wanatuhumiwa kuhusika katika mauaji hao.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya watu nne  Mustafa Badreddine, Salim Ayyash, Hussin Oneissi na Assad Sabra  ambao pia inasadikiwa kuwa ni wanacham wa kundi la Hezbollah kundi ambalo linashutumiwa kuhusika katika mauji ya Rafiki Hariri.

Hata hivyo kesi hiyo imeanza huku watuhumiwa kutokuwepo mahakamani na jaji David Re kuamua kuwa kesi itaendelea kwa "watuhumiwa kukana kosa hilo."

Rafiki Hariri, na watu wengine 22 waliuwawa mwaka 2005, baada  milipuko ya abomu kutoe katika eneo ambalo walikuwepo na kundi la Hezbollah kushutumiwa kuhusika na mauaji hayo, japo kundi hilo limekana  kuhusika na  mauaji hayo na pia kuipinga mahakama hiyo.

Hata hivyo baada ya kuuwawa kwa Hariri, jeshi la Syria lililazimika kuondoka nchini Lebanoni ambapo jeshi hilo lilikuwa likilinda amani nchi  Lebanoni.

Monday, January 13, 2014

FIFA ya Sepp Blatter yafanya alicho takiwa kupewa Pele.

FIFA ya Sepp Blatter yafanya alicho takiwa kupewa Pele.

Zurich, Uswizi - 13/01/2014. Edson Arantes Nascimento alimaarufu kama Pele, ametunukiwa zawadi maarumu ya mpira wa dhahabu  na kutambulika kuwa yeye  ndiye alikuwa mchezaji bora wa dunia katika karne 20 na mpa sasa hakuna ambaye amamesha wahi kuvunja rekodi yake ya usakataji wa soka na ufungaji wa magoli duniani kote hadi sasa.

Akiongea baada ya kupokea zawadi hiyo ya mpira wa dhahabu, ambao umeanzishwa kwa mara ya kwanza, Pele alisema "sasa naona ndoto yangu imekamilika, kwani nimekuwa na wivu kuona wengine wakitunukiwa na hivyo kwa sasa nina kombe vyote nilivyo kuwa navihitaji"

Sepp Blatter ambaye ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu FIFA akimsifu Pele alisema" Hakuna mchezaji ambaye amemfikia Pele katika historia ya mpira wa miguu duniani.
"Amefunga magoli zaidi ya alfu moja na kuwafanya watu wapende mchezo wa mpira wa miguu pote duniani na kwa uwezo wake wakusakata soka, na ni mchezaji wa karne ya 20"

Pele hakuweza kupata zawadi hii ya mpira wa dhahabu kwa kuwa mchezaji bora wa dunia enzi za uchezaji wake,  kwa sababu alikuwa hajawahi kucheza ligi za Ulaya japo alikuwa akitikisa dunia kwa umairi wake wa kusakata soka na kuwanyanyasa mabeki na makipa kugalagala na kurudi nyavuni kuotoa mpira ulio tikisa nyavu.


Cristiano Ronaldo atunzwa mpira wa dhahabu kwa mara ya pili.

Cristiano Ronaldo atunzwa mpira wa dhahabu kwa mara ya pili.

Zurich, Uswizi - 13/01/2014. Mchezaji wa Real Madrid  Cristiano  Ronaldo amechaguliwa kuwa mcheaji bora wa dunia wa mwaka 2013

Cristiano Ronaldo 28, amechaguliwa  kwa kura 1,365  na kuwashinda wachezaji wenzake wawili Lionel Messi  1,205 wa timu ya Barcelona. Na Frank Ribery 1,127 wa Buyen Munich ambao walifikia fainali katika uchaguzi huo.

Akiongea baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2013, Cristiano Ronaldo alisema, " sina cha kusema, na nawashukuru wachezaji wenzangu, uongozi kwa jumla, kwani kupata tunzo hili siyo rahisi."

Tuzo hili la kuwa mchezaji bora wa dunia litakuwa ni la mara ya pili katika maisha yake Cristiano Ronaldo ya kimpira kufuatia la kwanza alilopata mwaka 2008.Areal Sharon alazwa nyumba yake ya milele.

Areal Sharon alazwa nyumba yake ya milele.

Tel Aviv, Izrael - 13/01/2014. Mamia ya Waizrael wameudhuria mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu na amiri jeshi wa nchi hiyo Areal Sharon.

Mazishi ya waziri Areal Sharon yalifanyika katika shamba leke  kwenye eneo la jangwa la Negev.

Waziri mkuu wa sasa wa Izrael Benyamin Netanyahu ambaye aliongoza mazishi kwa niaba ya serikali, alisema " Sharon ni moja ya komanda wa Kiizrael ambao watakumbukwa kwa kuitete Izrael na Wajuishi "
Mazishi ya Areal Sharon yameudhuliwa na makamu wa rais wa Mareakani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergi Levrov, aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Brair na viongozi wengi kutoka sehemu tofauti duniani kasoro viongozi kutoka Afrika na Amerika ya Kusini.

Areal Sharon 85, alifariki kutokana na kuugua kwa  baadhi ya viongo vyake vya ndani ya mwili, na hii ilitokana hapo mwanzo wa mwaka 2006 kupata ugonjwa wa kiaharusi ambao ulimsababishia kulazwa kwa muda wa miaka saba.

Saturday, January 11, 2014

Waziri wa ulinzi wa Uingereza hausishwa na mateso wafungwa Irak.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza hausishwa na mateso ya wafungwa Irak.

London, Uingereza - 11/01/2014. Shirika la kutete haki za binadamu na katiba ya Ulaya lenye makao yake nchini Ujerumani limeiomba mahakama inayoshughulikia makaosa ya jinai ICC, kuchunguza matendo ya uvunjwaji wa haki za binadamu uliofanywa na viongozi wa serikali wa Uingereza.

Likiataja shirika hilo limesema "Geoff Hoon ambaye alikuwa waziri wa ulinzi na katibu mkuu  Adam Ingram kuwa walihusika kwanjia moja au nyingine katika mateso na mantendo yaliyo kuwa yanakuiuka haki za binadamu kati ya mwaka 2003 na 2008 na kuvunja sheria ya Geneva ya kulinda wafungwa wa kivita."

Hata hivyo watu hao ambao wanashukiwa kufanya makosa hayo wamekana kuhusika na makosa hayo.

Kesi hiyo ambayo ina kurasa 250,  ilikabidhiwa kwa ICC, huku ikiwa na makosa 85 ambayo inasemekana yamevunjwa  na viongozi hao, na hivyo kuomba wachunguzwe.

Wakati wa vita vya Irak, wanajeshi wa Uingereza walishutumiwa kwa kuhusika katika kutesa wafungwa wa kivita, ambapo Geof Hoon alikuwa ndiye mkuu wa wizara ya ulinzi ya nchi ya Uingereza.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael hatupo naye tena kimwili.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael hatupo naye tena kimwili.

Tel Aviv, Izrael - 11/01/2014. Wanachi wa Izrael wamekubwa na msiba mkubwa kufutia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu na amiri jeshi wa nchi hiyo kutokea leo hii.

Ariel Sharon 85, ambaye alikuwa amelazwa hospital kwa muda mrefu, baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi mwaka 2006  na ambapo  ulisababisha akupata madhara ndani ya viongo vya mwili wake na kupelekea kifo.

Shlomo Noy, ambaye ni msemaji wa hospital ambayo alikuwa amalazwa Sharon alisema " matibabu ya kila aina yalifanyika ili kummponya Sharon, lakini haikuwezekana na hivyo hatupo naye tena."

Msemaji wa familia ya Areal Sharon, Yoram Ravid amesema " kwa kuwa Sharon alikuwa ni mwanajeshi na hivyo naimani mazishi yake yafafanywa kwa taratibu za kijeshi."

Areal Sharon, atakumbukwa kwa hisia tofauti, kwa wengine kumwita shujaaa na wengine muuaji.

Kufuatia kifo cha Areal Sharon, Viongozi mbali mbali duniani wametuma salamu zao za rambi rambi kwa watu na serikali ya Izrael.

Friday, January 10, 2014

Risasi zalipuka baada rais Michel Djotodia kutagaza kuachia urais.

Risasi zalipuka baada ya rais Michel Djotodia kutagaza kuachia urais.


Bangui, Afrika ya Kati - 10/01/2014.  Rais wa mpito wa Afrika ya Kati ameachia madaraka baada ya serikali yake kushindwa kuhimili vishindo vya mvurugano wa kisiasa nchi humo.

Tangazo hilo la rais Michel Djotodia kuachia madaraka limetolewa, huku mkutano wa kuleta amani ukifanyika nchini Chad.

Baada ya kutangazwa kujiudhuru kwa Djotodia, milio ya risasi ilisikika katika sehemu tofauti jiji Bangui, na kambi ya wakimbizi  Kikiristu 100,000 iliiingiwa na nderemo, na huku hakukuwa na hata mmoja wa wapiganaji wanaomuunga mkono Djotodia mitaani.

Kufuatia habari za kujiudhuru Michel Djotodia, waziri Ufaransa Ulinzi wa Jean-Yves le Drian amesema " tunatarajia kuwepo na uongozi mpya ambao utaiongoza Afrika ya Kati hadi kipindi cha uchaguzi na kuunda serikali itakato ongoza nchi kwa  kufuata sheria."

Afrika ya Kati nchi ambayo ilikuwa koloni la Ufaransa, imekumbwa na mvurugo wa kisiasa ambao umepelekea kuleta matabaka ya kidini kati ya Waislaam na Wakristu ambayo  kwa sasa makundi hayo yanapigana.
Na tangu kuanza kwa vurugu za kisiasa nchini Afrika ya Kati,  maelfu ya watu wamesha poteza maisha, mali zao na hata kukimbia na kuchukua ukimbizi nje ya nchi ya Afrika ya Kati.

Thursday, January 2, 2014

Mwaka 2014 waanza kwa Wakenya kujeruhiwa na bomu.

Mwaka 2014 waanza kwa Wakenya  kujeruhiwa na bomu. Mombasa, Kenya - 02/01/2014. Mlipuko wa  bomu umetokea  baada ya watu walio kuwa kwenye pikipiki kurusha bomu katika hotel moja mjini Mombasa.

Akiongea kuhusu shambulizi hilo, Evans Achoki ambaye ni mkuu wa tarafa ya Kwale alisema " nilisikia mlipuko uliotokea katika hotel kwa jina Tandoori na baadaye nilipofika pale nilikuta watu wamejeruhiwa"

Kuthibitisha mlipuko huo, msemaji wa polisi Jack Ekakuro amesema " watu 10 wamejeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu na kwa sasa majeruhi wapo hospital kwa matibabu."

Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu, tangu nchi hiyo ilipoamua kulisaidia jeshi la serikali ya Somalia katika harakati zake za kupambana na kund la Al Qaeda. Na kundi hilo la al Qaeda kuhaidi kufanya mashambulizi nchini Kenya.

Mwaka 2013 haukuwa mwaka wa heri kwa Wairak.


New York, Marekani 02/01/2014. Umoja wa mataifa umetoa taarifa kuwa mwaka 2013 umekuwa mwaka ambao mauji kwa Wairak yalizidi kulinganishwa na miaka ya nyuma nchi humo.

Ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa "watu wapatao 8,868  wamepoteza maisha yao, na mauaji ya kutisha yametokea mwezi wa Desemba 2013 ambapo watu 759 ambapo 69 kati yao walikuwa ni walinzi na  maafisa usalama wa taifa."

Mauaji mengi yanayo tokea nchini Irak yamekuwa ni ya kisiasa au ya kimakundi  ambayo yanahusisha Washia na Wasuni, ambapo wamekuwa wakivutana katika  kuongoza nchi,  tangu kuangushwa kwa utawala wa Saadam Hussein na jeshi la Marekani na washiriki wake miaka 10 iliyopita.

Wednesday, January 1, 2014

Hali ya afya ya waziri mkuu wa zamani wa Izreal ipo tete.

Hali ya afya ya waziri mkuu wa zamani wa Izreal ipo tete.

Jerusalemu, Izrael 01/01/2014. Afya ya aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael, Ariel Sharon inazidi kudorola siku hadi siku toka alipofanyiwa upasuaji wa na kuwekewa mirija ya kupitishia chakula mwezi Septemba mwaka jana.

 Amir Marom, ambaye ni msemaji wa hospital ya Hashomer alipo lazwa Sharon alisema kuwa " nikweli hali ya Sharon siyo nzuri kiafya na madakitari bado wapo wanafuatilia afya yake kwa ukaribu."

Kwa mijibu wa habari zinasema kuwa hali ya afya ya Ariel Sharoni ilianzakudhoofika  mara baada ya viungo vyake vya ndani ya mwili  kushindwa kufanya kazi vizuri. Lakini hazikueleza lini matatizo hayo yaliianza.

Waziri mkuu Arel Sharon 85 ambaye ni mwanzilishi wa chama cha Kadima, alilazwa hospital tangu mwaka January 4, 2006, baada ya kupata ugonjwa wa kiharusi, ambao ulimsababishia kutoka katika ulingo wa siasa nchi Izrael. 

Balozi wa Palestina auwawa kwa bomu.
Prague, Czecheslovakia - 01/01/2014. Balozi wa Palestina nchini  Czecheslovakia, ameuwawa kwa  bomu kwenye jengo analo ishi katika jiji la Prague.

Akithibitisha kuwepo na mlipuko wa bomu, msemaji wa polisi Andrea Zoulova amasema "balozi Jamal al Jamal   alifariki mara baada ya kufikishwa hospitali"

Na habari kutoka kwa ofisi ya mambo ya nje ya nchi  ya Wapalestina imesema " mlipuko wa bomu ulitokea wakati balozi, Jamal al Jamal alipo kuwa akijaribu kufungua kabati iliyokuwa imeletwa kutoka ofisi za zamani za ubalozi huo"

Hata hivyo serikali ya nchi Czechslovakia haija thibitisha kuwa mlipuko huo unahusika na ugaidi.Tuesday, December 31, 2013

Jeshi la serikali la rais Salva Kiir lazidiwa nguvu.

Jeshi la serikali la rais Salva Kiir lazidiwa nguvu.


Bor, Sudani ya Kusini - 31/12/2013. Wapiganaji wanao pingana na  serikali ya Sudan Kusini, wa mekamata  mji wa Bor, baada ya kupambana vikali na  wajeshi wa serikali na kulizidi nguvu.

Akiongea baada ya kuukamata mji huo,  Moses Ruai ambaye ni msemaji wa jeshi la upinzani amesema " Mji wa Bor upo mikononi mwetu, na hivyo makao makuu wa jimbo la Jonglei ni yetu pia."

Wakati mapambano yanaendelea, kiongozi wa upinzani  na ambaye jeshi lake limetwaa mji wa Bor Riek Machar amekataaa kukutana na rais Salva Kiir ili kufanya mazungumzo ya kuleta amani ambayo yalitarajiwa kufanyika jijini Addis Ababa Ethiopia hii karibuni.

Hata hivyo kwa upande wa serikali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan ya Kusini, Barnaba Marial Benjamin, amesema " mpango wa Riek Machar kushirikiana na kugawana madaraka na rais Salva Kiir haupo tena, na hii ni kutokana na kuwa Machar ni kiongozi wa jeshi linalotaka kupindua serikali halali ya wanchi wa Sudan ya Kusini."

Tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe,  kwenye nchi changa ya Sudan ya Kusini na ambayo ilipata uhuru wake 2011, watu wapatao 1000 wamesha poteza maisha yao, wengi kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa kutokana na vita hivyo.

Urusi ya shutuliwa na milipuko ya mabomu mfululizo.


Urusi ya shutuliwa na milipuko ya mabomu  mfululizo.

Moscow. Urussi - 31/12/2013. Muuaji ya kigaidi yametolea tena kwa mara ya pili katika mji wa Volgograd na kuuwa watu wapatao 14 na wengi 41 kujeruhiwa vibaya ja.

Mauji hayo yalitokea baada ya  bomu kulipuka katika basi la abiria linalo fanya mizinguko ya kuchukua abiria katika mji huo na kuwashitua wananchi wengi wa Urussi ambapo nchi yao ipo mbioni kuandaa mashindano ya michezo ya Olympic Baridi siku chache zijazo.

Mlipuko wa bomu  ndani ya basi umefuatia mlipuko mwingine ambao umetokea siku moja katika kituo cha treni cha mji huo na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya muuaji wa kujitolea muhanga kusimamishwa katika kizuizi cha kuingilia katika kituo hicho.

Kufuatia milipuko hiyo katika mji wa Volgograd, rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza ulinzi uongezwe na kuhaidi kuwa wale wote ambao wanahusika na milipuko hiyo ambayo ina nia ya kutishia wananchi wa Urusi watatiwa nguvuni na sheria itapitisha panga lake kwao.

Friday, December 27, 2013

Rais wa Sudan ya Kusini akubali suruhu.

Rais wa Sudan ya  Kusini akubali suruhu.

Juba, Sudan ya Kusini - 27/12/2013. Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir  amekubali kusimamishwa mapambano ya kivita kati yake na kundi ambalo linaunga mkono mpinzani wake Riek Machar ambaye alikuwa makamu wake wa urais.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  na waziri mkuu wa Ethiopia  Hailemariam Desalegn waliweza  kumshawishi rais Kiir kukubali kusimamishwa kwa vita baada ya kukutana na kujadiliana katika mji mku  wa Juba.

Akiongea  baada ya rais Kiir  kukubali kusimamishwa kwa vita , rais Uhuru Kenyatta amaesema " nimefurahishwa na kitendo cha rais Kiir kukubali kusimamisha vita, kwani nafasi iliyopo ni finyu, na naomba ijulikane kuwa  IGAD haitaruhusu kuona rais aliyechaguliwa kihalali anatolewa madarakani kwa nguvu"

" Na nawaomba Riek Machar na rais Salva Kiir  kuhakikisha amani inarudi nchini Sudani ya Kusini kwani vita siyo suruhu ya kuleta maendeleo ya nchi." Aliongeza  rais Uhuru Kenyatta.

Jitihada za kusimamisha vita nchini Sudan ya Kusini  zinasimamiwa na  (Inter-Government Authority on Develoment -IGAD) ikiwa  na nia ya kusimamia uongozi bora na kuhakikisha kuondoa migogoro ya kisiasa katika nchi zilizopo  Afrika ya Mashariki na Kati.

Mvutano kati ya Udugu wa Kiislam na serikali waiweka amani ya Misri njia panda.


Kairo, Misri -27/12/2013. Waandamaji wanaounga mkono kundi la Undugu wa Kiislaam ( Muslim Brotherhood) wamepambana polisi katika matukio tofauti yaliyo tokea nchi Misri tangu kutangazwa kuwa kudi hilo ni kundi la kigaidi nchi Misri.

Katika maandamano hayo watu watatu wamepoteza maisha jiji Kairo, na wengine kujeruhiwa vibaya wakati polisi wa kuzuia ghasia  walipo pambana na waandamanaji,  na zaidi ya watu 265 wamekamatwa kutokana na vurugu hizo,  

Tangu kutolewa madarakani kwa nguvu kwa rais Mohammed Morsi, hali ya amani na utulivu imechafuka nchini Misri, na hii inatokana na wanachama  wanaounga mkono kundi la Undugu wa Kiislaam kutaka rais Mohammed Morsi arudishwe madarakani na pia wanapinga kitendo cha serikali kukitangaza cha chama cha Udugu wa Kislaamu kuwa cha kigaidi.

Saada al Hariri alia na Hezbollah.

Beiruti, Lebanon - 27/12/2013.  Saad al Hariri ambaye alisha wahi kuwa waziri mkuu wa Lebanoni, amelilaumu kundi la Hezbollah kwa kuhusikia na shambulizi la bomu ambalo limemuua mmoja ya mshauri wake mkuu.

Mohamad Bahaa Chatah 62, aliuwawa baada bomu kulipuka  katikati ya msafara wake wakati  alipo karibia ofisi za majengo ya serikali ambapo alikuwa njiani keelelea kwenye mkutano wa kuipinga Syria uliyokuwa ukiongozwa na Saad al Hariri

Mlipuko huo pia uliharibu majengo na kusababisha baadhi kushika moto na kuungua vibaya.

Akiongea kuhusu mauaji ya Chatah, Saada al Hariri alisema " watu walio muua Chatah ni wale ambao wanataka haki isitendeke kufuatia kuwepo na kesi inayotarajiwa kuanza kwenye koti ya kimataifa mjini  Hague Uholanzi mapema mwezi January 2014."

Mohamad Chatah, alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya Syria,  amekuwa akipinga na kulaumu kundi la Hezbollah kwa kushirikiana na rais Bashar al Assad katika vita vinavyo endelea nchi Syria.

Kifo cha Chatah kimekuja wiki tatu kabla ya kuanza kesi zidi ya baadhi ya wanachama wa Hezbullah ambao wanasadikiwa kuhusika katika mauaji ya  mwaka 2005 ya waziri mkuu wa Lebanoni  Rafik al Hariri ambaye ni baba wa Saad al Hariri,